Je, serikali ya Kenya inapanga kuminya uhuru wa maandamano?

  • | BBC Swahili
    2,724 views
    Mbunge wa jimbo la Nairobi Esther Passaris amependekeza mswada mpya ambao utabadilisha kikamilifu jinsi maandamano yanavyoendeshwa nchini Kenya. Muswada wa sheria ya marekebisho ya mfumo wa umma wa 2025 unapendekeza mabadiliko katika sheria iliyopo ya Mfumo wa Umma (Sura ya 56) kwa kuweka vikwazo vya mikusanyiko kwenye maeneo ya mikutano ya hadhara. Mapendekezo ya Passaris yameibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi wakiyapinga.