Je, unajua sababu zilizopelekea Putin kuhamisha silaha za nyuklia Belarus?

  • | VOA Swahili
    10,648 views
    Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye mpaka na Belarus wametumia ndege zisizo kuwa na rubani ili kufuatilia aina yoyote ya uchokozi unaofanywa dhidi yake na Russia. Kuna habari zinazoeleza Rais wa Russia Vladimir Putin anapanga kupeleka silaha huko Belarus bila ya kukiuka majumu yake ya kimataifa ya kutosambaza silaha za nyuklia. Ungana na mwandishi wetu akikueleza hatua ambayo Russia inachukua ya kupeleka silaha kali na kutoa mafunzo ya kuzitumia huko Belarus. Endelea kusikiliza... #wanajeshi #ukraine #belarus #ndege #uchokozi #russia #silaha #vladimirputin #voa #voaswahili #dunianileo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.