Jinsi msongamano wa malori eneo la Busia imekuwa donda sugu kwa madereva wa masafa marefu

  • | Citizen TV
    907 views

    Kwa muda mrefu sasa, swala la msongamano wa malori ya masafa marefu katika miji ya mpakani ya Busia na malaba limekuwa donda sugu, huku shughuli za usafiri zikiathirika pakubwa katika miji hiyo. Milolongo ya malori ya kubeba bidhaa za petroli na yale ya mizigo ambayo hufikia hadi urefu wa zaidi ya kilomita 10 kutoka mpakani hushuhudiwa eneo hili.