Juhudi za kuimarisha utoshelevu wa chakula katika Kaunti ya Bungoma zimepigwa jeki kupitia mpango wa kuwawezesha wananchi kwa ufugaji wa kuku, unaolenga makundi yaliyo katika mazingira magumu katika jamii.
Jumla ya makundi 150 yanayojumuisha wanawake, vijana na watu wanaoishi na ulemavu yanatarajiwa kunufaika na vifaa vya ufugaji wa kuku ili kuboresha uthabiti wao wa kiuchumi. Haya ni kwa mujibu wa shirika moja la kilimo linalofanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Bungoma wakati wa mafunzo ya siku nne ya kuwapa ujuzi wa kisasa wa kilimobiashara. Mafunzo hayo yanawezesha makundi kutoka maeneo ya Kanduyi, Bumula na Sirisia kupata ujuzi wa biashara ya kilimo.