Jumla ya wabunge 282 wapiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumuondoa naibu rais Rigathi Gachagua

  • | Citizen TV
    800 views

    Jumla ya wabunge 282 jana walipiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumuondoa ofisini naibu wa rais Rigathi Gachagua. Wabunge wengine 44 walipiga kura ya kupinga mswada wa kumuondoa mamlakani. Zoezi hilo la kupiga kura liliandaliwa mwendo wa saa tatu usiku baada ya siku nzima ya kusikiza kauli za wabunge dhidi ya naibu rais.