Skip to main content
Skip to main content

Kaikai awataka wanafunzi wa Maasai Mara kuzingatia maadili ya uandishi wa habari

  • | Citizen TV
    334 views
    Duration: 1:33
    Mkurugenzi wa Uhariri wa Kampuni ya Royal Media Services, Linus Kaikai, amewahimiza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara kuzingatia maadili, uwajibikaji na uadilifu wanapojianaa kuwa wanahabari. Akizungumza katika kongamano lililowaleta pamoja wanafunzi na wahadhiri wa idara ya mawasiliano katika chuo hicho huko Narok, Kaikai alisema kuwa wanahabari wanastahili kuwa wenye maadili ya kuigwa na kuongeza kuwa uwajibikaji ni moja wapo ya mihimili ya tasnia ya uanahabari ambayo inachangia imani ya umma na heshima.