- 236 viewsDuration: 2:44Kamati ya bunge kuhusu elimu leo imemshutumu katibu wa elimu Julius Bittok kwa utepetevu na kususia vikao vya kamati hiyo mara kwa mara bila sababu. Wanakamati hao sasa wanasema Bittok amekuwa kizingiti katika utendakazi wao. Aidha wameitaka tume ya tsc kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliokamilisha elimu ya msingi na sekondari wanapokea vyeti vyao mara moja hata ikiwa wana madeni ya karo.