Kamati ya bunge yatathmini uhalibifu wa barabara eneo la Mwea

  • | Citizen TV
    204 views

    Kamati ya bunge kuhusu uchukuzi na miundomsingi imetoa hakikisho kuwa serikali itakarabati au kujenga upya Barabara, madaraja na miundomsingi nyingine iliyoharibiwa na mafuriko humu nchini. Akizuru eneo la Kandongu huko mwea , kaunti ya Kirinyaga, mwenyekiti wa kamati hiyo George Kariuki, amesema kuwa zaidi ya kilomita 560 za barabara zitajengwa katika eneo la mradi ya unyunyizaji maji la mwea ili kuimarisha miundomsingi itakayosaidia ukulima wa mpunga. zaidi ya watu 600 kaunti ya Kirinyaga wameathriika na mafuriko. mafuriko hayo pia yameathiri shule eneo la mwea.