- 754 viewsDuration: 2:54Kamati maalum ya kushughulikia fidia kwa waathiriwa wa maandamano imeanza rasmi kazi baada ya wanakamati kula kiapo hii leo. Kamati hiyo inayoongozwa na mshauri wa rais kuhusu sheria Profesa Makau Mutua, imesisitiza kwamba itahakikisha familia za waathiriwa pamoja na maafisa wa polisi walioathirika wamepata fidia. Rais wa Chama cha mawakili Faith Odhiambo, ametetea kuhusika kwake na kamati hiyo licha ya kukashifiwa na wakenya kwenye mitandao.