- 7,860 viewsDuration: 3:11Kampeni zimekamilika rasmi katika eneo bunge la Ol Kalou, Kaunti ya Nyandarua, ambapo wagombea mbalimbali walijitokeza kuuza sera zao katika dakika za lala salama kabla ya uchaguzi wa Alhamisi. Wagombea wa vyama vya UDA na DCP waliandaa mikutano ya hadhara mjini Ol Kalou kuwashawishi wapiga kura, wakiahidi kuchapa kazi endapo watachaguliwa. Wakati huo huo, Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, amesema usalama utaimarishwa ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.