- 184 viewsDuration: 2:11Serikali ya kaunti ya Kwale imesema imeshirikisha kampuni 400 za makundi ya akina mama na vijana kufanya biashara na serikali hiyo baada ya kuwezeshwa na kupewa mafunzo ya usimamizi wa biashara. Akizungumza katika uzinduzi wa basi la kikundi cha Mwajambo ambacho ni cha hivi karibuni kuunda kampuni, waziri wa biashara na utalii kainti hiyo Michael Mutua amesema kampuni hizo zinapewa kandarasi za ujenzi wa hospitali na shule za chekechea pamoja na usambazaji vifaa tofauti miongoni mwa kandarasi nyingine.