Viongozi wa Kanisa Katoliki wameendelea kuwarai vijana kudumisha amani miezi 13 kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa.
Maskofu wa Kanisa Katoliki, waliowajumuisha wawakilishi kutoka mataifa 11 ya Afrika Mashariki, walikutana na vijana jijini Nairobi na kuwaonya dhidi ya kutumiwa kuendeleza migawanyiko ya kisiasa. Pia wamewahimiza kuepuka vurugu na kutafuta suluhu kupitia mazungumzo. Zaidi ya vijana elfu kumi kutoka mataifa ya Afrika Mashariki wanashiriki kongamano hilo la siku nane, linalofanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne.