Kanisa la Glory of Christ laondolewa kwenye sajili baada ya kiongozi wake kukemea utekaji nyara

  • | Citizen TV
    16,161 views

    Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeondoa kwenye sajili ya makanisa kanisa la Christ Church – ufufuo na uzima pamoja na matawi yake 2000, linalomilikiwa na mbunge wa Kawe na askofu Josephat Gwajima. Hii ni baada ya mhubiri huyo kupinga utekaji nyara na kutoweka kwa watu nchini Tanzania. Serikali ikisema mahubiri ya askofu Gwajima yana nia ya kuchochea wananchi dhidi ya serikali na kuhatarisha amani.