Skip to main content
Skip to main content

Katibu wa afya ya umma ashauri wanahabari kuangazia taarifa chanya

  • | Citizen TV
    212 views
    Duration: 1:19
    Katibu katika Idara ya Afya ya Umma Mary Muthoni amewataka wanawake katika vyombo vya habari kuangazia taarifa zenye athari zitakazowahamasisha wanawake wengine kujitokeza na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Akizungumza jijini Nairobi wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyoandaliwa na chama cha Uhusiano mwema wa Umma cha Kenya, Muthoni alisema wanawake wanapaswa kusimulia hadithi za wanawake waliobadilisha jamii ili kuhamasisha wengine. Hafla hiyo iliwahimiza wanawake kupigania nafasi za uongozi, si kuwa watekelezaji pekee bali washiriki wa kufanya maamuzi.