- 3,465 viewsDuration: 3:42Uhusiano wa Rais William Ruto na aliyekuwa wakili wake Katwa Kigen ulijitokeza katika kikao cha kuwahoji majaji wanaotaka wadhifa wa jaji wa Mahakama ya Upeo. Jaji Kigen akijitetea dhidi ya tetesi kuwa huenda akawa na mapendeleo iwapo atafaulu na iwapo kutakuwa na kesi ya kupinga matokeo ya urais baada ya uchaguzi. Jaji huyo pia ametetea hatua yake ya kutuma ombi la kujiunga na Mahakama ya Upeo miezi mitatu tu baada ya kujiunga na Mahakama ya Rufaa. Wengine waliofika mbele ya Tume ya JSC ni aliyekuwa mwenyekiti wa IPOA Anne Makori na Jaji wa Mahakama Kuu Joseph Sergon.