Kaunti ya Bungoma kuajiri madaktari na wauguzi mia mbili

  • | Citizen TV
    319 views

    Kaunti ya Bungoma inaajiri madaktari na wauguzi mia mbili kama njia mojawapo ya kuimarisha huduma za afya kaunti hiyo. Kulingana na waziri wa afya Dkt. Andrew Wamalwa hatua hiyo imearifiwa na uhaba wa madaktari katika kaunti hiyo. Aidha inaaminika kuwa kuajiriwa kwa wauguzi hao na madaktari kutawasaidia wangojwa ambao wamelazimika kusafiri mbali kutafuta matibabu. Madaktari hao pia wataimarisha kiwango cha afya ya msingi kwa wakaazi katika pana la magharibi.