Kaunti ya Kilifi imeanzisha uhamasisho kwa wakazi kuhusu mabadiliko ya tabianchi

  • | Citizen TV
    242 views

    Serikali ya kaunti ya Kilifi imeanzisha kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga katika maeneo ya mashinani ili kusaidia kukabiliana na changamoto zaidi. Lengo la kampeni hiyo ni kutoa mafunzo kwa wakazi katika wadi zote 35 kuhusu njia bora za kubuni miradi endelevu ya kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya anga. Afisa Mkuu katika idara ya Uvuvi Zamzam Ali amesema idara yake imeanza kutoa mafunzo kwa wakaazi wa wadi 14 katika Kaunti Ndogo tatu. Mpango mzima ni kusaidia miradi ambayo inahusu mabadiliko ya hali ya anga kama vile kupanda mikoko, na kuongeza misitu.