- 488 viewsDuration: 1:25Kenya imejiandaa kuongoza ulimwengu katika kuadhimisha Mwaka wa Kimataifa wa maafisa wa kujitolea kwa ajili ya Maendeleo endelevu 2026. Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kongamano hilo katika jengo la Umoja wa Mataifa huko Gigiri, Nairobi, Katibu wa idara ya maslahi ya Jamii na Masuala ya Wazee, Joseph Motari alisisitiza mageuzi makubwa ambayo yanaiweka Kenya katika nafasi ya jukumu hili la uongozi, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Jamii 2025 na Sheria ya Watu Wenye Ulemavu 2025.