Kenya na Korea Kusini kuimarisha mahusiano

  • | KBC Video
    26 views

    Kenya imejitolea kuimarisha uhusiano wake wa kibiashara na Korea Kusini katika juhudi za kupiga jeki nafasi za biashara na uchumi katika mataifa haya mawili. Rais William Ruto aliyekutana na mjumbe maalum wa rais wa Korea Kusini pamoja na naibu waziri wa kwanza wa mashauri ya nchi za kigeni nchini humo, Hong Kyum Kim, katika ikulu ya Nairobi alikariri thamani ambayo taifa hili linaweka katika ushirikiano wake na Korea Kusini. Alisema ushirikiano huo unalenga kustawisha taasisi za mafunzo ya kiufundi na anuwai-TVET humu nchini na sekta za afya ya umma, maji, usafi pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive