- 333 viewsSerikali imekiri kuwa Kenya inafanya mazungumzo na serikali ya Marekani kuhusu mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola. Waziri wa Afya Aden Duale hata hivyo hakuthibitisha wala kukataa ripoti kuwa Marekani inajenga kituo cha matibabu ya kudhibiti virusi nchini, kitakachowahudumia raia wa Marekani pekee. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, serikali ya Uganda imetangaza kufunga mpaka wake na taifa la DR Congo.