- 3,408 viewsDuration: 3:10Ubalozi wa Marekani hapa Nairobi umepuuzilia mbali madai kuwa data za wakenya na sampuli za wagonjwa zitasambazwa kiholela kwa serikali ya Marekani kufuatia kutiwa saini kwa mkataba kati ya nchi hizo mbili. Mwakilishi wa serikali ya Marekani nchini Susan Burns amesema kuwa mkataba wa ushirikiano wa afya uliotiwa saini na rais William Ruto na waziri w amasuala ya kigeni wa Marekani Marc Rubio jijini Washington, D.C. unalenga kufanikisha mipango mbalimbali ya afya nchini.