Kenya yaungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya uhuru wa uanahabari

  • | K24 Video
    55 views

    Kenya imeungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya uhuru wa uanahabari huku wito ukiwa wa kuboresha mishahara ya wanahabari, kukabiliana na mashambulizi dhidi ya wanahabari kutoka kwa asasi za usalama na kukomesha vitisho kutoka kwa maafisa wa serikali miongoni mwa changamoto nyingine. Maudhui ya mwaka huu ni ‘uanahabari wakati wa janga la mazingira, na wanahabari kutoka sehemu tofauti nchini wameshiriki matembezi ili kuhamasisha wakenya kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.