Pacha Grace Nyanjau na Mercy Nyambura, waliopata alama 52 na 47 mtawalia kwenye tathmini ya KJSEA bado hawajafanikiwa kujiunga na sekondari ya juu kwasababu ya kukosa pesa za karo na mahitaji mengine.
wanafunzi hao wawili wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya karo tangu walipokuwa katika shule ya msingi ya Karunga, mama yao akiugua ugonjwa w amoyo huku baba yao akifanya kazi za sulubu kijijini. aidha mama yao, Fidelis Wambui hana uwezo wa kufanya kazi kutokana na hali yake ya afya na amekuwa akitegemea hisani ya wanakijiji. Wanafunzi hao walioteuliwa kujiunga na shule za kutwa huko Murang'a na Kiambu wameshindwa kupata shilingi elfu 100 zinazohitajika kugharamia karo ya muhula huu na sare za shule.