Kesi mbili zinazopinga sheria za bima zasikizwa

  • | Citizen TV
    330 views

    Kesi mbili zinazopinga sheria ya bima ya afya ya jamii, sheria ya afya ya kimsingi na sheria ya huduma za kidijitali za afya inaendelea katika mahakama kuu mbele ya majaji Alfred Mabeya, Robert Limo na Freda Gathiru Mugambi. mawakili wa mashirika yanayopinga sheria hizo wanasema kuwa zinakiuka katiba na haki za kimsingi za wakenya. kesi hiyo imewasilishwa na Joseph Enock Aura, KMPDU, muungano wa wafanyikazi wa umma, muungano wa People’s Health Movement na chama cha wachuuzi.