- 9,540 viewsDuration: 3:55Mmoja wa vijana wawili waliopigwa risasi katika eneo moja la burudani, Kitengela ameaga dunia. Kevin Maseri, alifariki mapema leo akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi alikohamishwa kutoka hospitali ya rufaa ya Kajiado. Haya yamejiri huku polisi Kajiado wakithibitisha kupokea bunduki tatu kutoka kwa washukiwa na tayari watu 10 wameandikisha taarifa