- 6,036 viewsDuration: 2:28Kizaazaa kilishuhudiwa katika shule ya upili ya wasichana ya njoro kaunti ya nakuru baada ya wakaazi kuandamana kulalamikia kifo cha mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo. Familia ya Brenda akinyi, inasema mwana wao alifariki alipokuwa akitibiwa, ila wanasema alikuwa amewaeleza wasimamizi wa shule hiyo kuhusu maumivu ila hakupata usaidizi.