Kikundi cha Eselenkei Kajiado kimepata shilingi milioni nane kwa kutunza mazingira.

  • | Citizen TV
    328 views

    Kikundi cha Eselenkei Kajiado kusini kilicho na wanachama zaidi ya 3,000 kimefaidika na shilingi milioni nane kwa kutunza mazingira. Kikundi hicho kimetia saini mkataba wa makubaliano na shirika la Soil for the Future Afrika kuhakikisha kuwa wanatunza nyasi na miti ili kuimarisha uzalishaji wa hewa ya kaboni kwenye mazingira.