Skip to main content
Skip to main content

KILIFI KUANDAA MAADHIMISHO YA KIMATAIFA YA SIKU YA HALI YA JANGWA NA UKAME DUNIANI

  • | KNA Video
    34 views
    Duration: 1:55
    Kaunti ya Kilifi itakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Hali ya Jangwa na Ukame Duniani yanayofanyika Juni 17, huku wadau wa mazingira wakisisitiza umuhimu wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo kame. Katibu wa Idara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mhandisi Festus Ng’eno, amesema maadhimisho hayo yataangazia urejeshaji wa nyanda za malisho, uhifadhi wa mazingira, na njia za kuimarisha usalama wa chakula katika maeneo yanayokumbwa na ukame. Wadau pia wamejadili changamoto za migogoro kati ya binadamu na wanyamapori pamoja na uhaba wa maji safi katika baadhi ya maeneo ya Ganze na Kaloleni. Serikali na washirika wake wanatarajia kutumia hafla hiyo kuhamasisha suluhu endelevu za kukabiliana na ukame na uharibifu wa ardhi.