- 277 viewsDuration: 3:48Kilimo cha mpunga katika eneo bunge la Budalangi katika kaunti ya Busia kinatarajiwa kuimarika maradufu baada ya ujio wa teknolojia ya kupanda mmea huo kwa kutumia mashine ya kupandikiza. Kinyume na awali, mpunga unapandwa katika teo zinazowekwa kwenye kiota cha wavu wa kivuli kwa siku ishirini na moja kabla ya kuhamishiwa shambani na kupandwa kwa kitumia mashine ya kupandikiza.