- 81 viewsKilimo cha mrehani unaojulikana kwa lugha ya Kiingereza kama basil kimeanza kushika kasi katika maeneo kame nchini. Katika eneo la Kamulu, mkulima mmoja anakuza viungo vya mrehani ndani ya kivungulio akilenga masoko ya kigeni. Kwenye Kilimo Biashara jioni ya leo, mwanahabari wetu Denis Otieno anaangazia kilimo hiki kinachothibitisha kuwa hata mazao madogo yanaweza kufungua milango ya masoko ya kimataifa.