Katika eneo la Kaler, jamii iliyoko katika kaunti ndogo ya Nyatike ambayo hapo awali ilijulikana kwa kiangazi na ukame, mabadiliko yenye athari kubwa yanaendelea kushuhudiwa. Mahali ambapo hapo awali kulikuwa na mashamba yaliyokauka kwa jua na yasiyo na uhai, sasa kuna mashamba yaliyo na rangi ya kijani kibichi yanayonawiri, hata miezi kadhaa baada ya mvua ya mwisho kunyesha. Kufuatia ukame uliokithiri ,wakulima wa eneo hilo wamechukua hatua kwa kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji ya mvua, kwa ajili ya matumizi wakati wa vipindi virefu vya kiangazi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive