Kinara wa Azimio Raila Odinga adai Ruto anakataa ushauri

  • | K24 Video
    48 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga sasa anasema wakenya wasitarajie chochote kizuri kutoka kwa serikali ya kenya kwanza hasa kuhusu gharama ya maisha. Raila ameshikilia kuwa serikali imekataa kusikiza ushauri kuhusu. Jinsi ya kupunguza gharama ya maisha na badala yake kuongeza ushuru licha ya kuwa taifa limekuwa likikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Kinara huyo aliyekutana na wanafunzi wa vyuo vikuu katika wakfu wa Jaramogi Oginga Odinga, JOOF, anadai kuwa mkataba wa ununuzi wa mafuta kati ya serikali na serikali haujasaidia katika kupunguza bei ya petroli. Viongozi wa vyuo vikuu wametakiwa kuwa na misimamo na wasikubali kutishwa na serikali.