Kinara wa ODM Raila Odinga awataka wakaazi wa Wajir kujisajili chamani

  • | Citizen TV
    489 views

    Kinara wa ODM Raila Odinga leo anaendeleza mchakato wa kuandikisha wanachama wapya katika kaunti ya Wajir. Odinga anawataka wenyeji wa kaunti hiyo kuandikisha wanachama zaidi kwani ni baadhi ya kaunti zilizoandikisha wanachama wachache katika sajili ya ODM. Odinga amendamana na gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi na naibu vinara wa ODM Hassan Joho na Wycliffe Oparanya.