Skip to main content
Skip to main content

Kindiki amtaka Uhuru kuacha kuingilia utendaji wa serikali

  • | Citizen TV
    1,187 views
    Naibu Rais Kithure Kindiki amemtaka Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kukoma kuingilia masuala ya utendaji wa serikali, akisisitiza kuwa serikali inaendelea na ajenda yake ya kuboresha maisha ya wananchi. Akizungumza katika Kaunti ya Kwale County, Kindiki ametetea rekodi ya Rais William Ruto akisema kuwa ameonyesha maendeleo katika kuboresha hali ya maisha ya Wakenya. Aidha, amekashifu madai ya njama ya wizi wa kura, akieleza kuwa ana imani kuwa tume ya uchaguzi IEBC itaendesha uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika.