Skip to main content
Skip to main content

Kirinyaga: Watu 3 wafariki, wengine 3 wajeruhiwa kwenye Ajali

  • | Citizen TV
    3,136 views
    Duration: 1:02
    Watu watatu wameuawa na wengine watatu kuwachwa na majeraha baada ya magari mawili kugongana na bodaboda eneo la Mwea kaunti ya Kirinyaga. Inaripotiwa kuwa ajali hii ilitokea baada ya magari mawili yaliyobeba miraa yalipokuwa yakiendeshwa kwa kasi kugongana na bodaboda kwenye eneo la Makutano. Miongoni mwa waliofariki ni dereva wa moja wa gari hilo lililokuwa likitoka Ngurubani kuelekea Makutano. Watatu waliojeruhiwa walikimbizwa kwa matibabu kwenye hospitali zilizo karibu. Wakaazi wa eneo hilo sasa wakitaka polisi kudhibiti kasi za magari yanayobeba miraa na hata kuhakikisha upanuzi wa barabara