- 37,197 viewsDuration: 28:10Wabunge wa Bunge la Tanzania leo wamemaliza rasmi viapo vyao, hatua inayowafanya kuwa wabunge kamili na kuhitimisha kipindi cha kuwa wateule. Zoezi hilo lilianza jana na kukamilika leo katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. Baadhi ya wadau hata hivyo wanadai Bunge hili la 13 linaweza kukosa upinzani imara kutokana na idadi kubwa ya wabunge kutoka chama tawala CCM. Tumezungumza na baadhi ya wabunge walioapishwa kuhusu matarajio yao. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw