- 312 viewsDuration: 2:37Kituo cha kutoa mafunzo kuhusu ugonjwa wa Ebola kimezinduliwa rasmi jijini Mombasa huku wahudumu wa afya wakianza kupokea mafunzo ya jinsi ya kudhibiti mlipuko endapo maambukizi yataripotiwa. Maafisa wanaosimamia shughuli hiyo wanasema kituo hicho kimewekewa vifaa muhimu vya kutenga na kuhudumia watu wanaoonyesha dalili za ugonjwa wa Ebola. Wamesisitiza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya kuimarisha utayari wa sekta ya afya kukabiliana na tishio lolote la mlipuko wa Ebola.