Kizaazaa chashuhudiwa nje ya ofisi ya gavana Meru

  • | Citizen TV
    2,778 views

    Baadhi ya wakaazi wa meru wamekabiliana na polisi kwenye maandamano wakimtaka Gavana Kawira Mwangaza kuondoka afisini, baada ya kung’atuliwa mamlakani. Wakaazi hawa ambao walifunga barabara inayoelekea kwenye afisi za gavana na kuwasha moto kwenye barabara hiyo walimtaka mwangaza kuondoka, wakisema aling’atuliwa sheria zote zikifuatwa na hana msingi wowote kuwa afisini. Maandamano haya pia yalifanyika katika maeneo ya maua na nkubu, wakaazi hawa wakiahidi kurejea kufunga afisi hizo kesho kama mwangaza atafika afisini.