Kongmano la UNEA-6 litafanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 26 Februari – 1 Machi

  • | TV 47
    6 views

    Kongamano la sita la Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-6) litafanyika kuanzia tarehe 26 Februari hadi 1 Machi katika makao makuu ya mpango wa mazingira wa umoja wa mataifa (UNEP) jijini Nairobi, Kenya.

    Kongamano hilo limetanguliwa na kikao na wanahabari, ambacho kitasaidia kuweka msingi wa kongamano linalotarajiwa.

    Shirika la UNEP, pamoja na serikali ya Kenya inanuia kuangazia masuala mbalimbali ya mazingira pamoja na masuala muhimu ya kujadiliwa katika UNEA-6.

    Bi. Inger Andersen, Mkurugenzi Mkuu wa UNEP, Soipan tuya, Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu nchini Kenya pamoja na Bi. Radhika Ochalik, Mkurugenzi, Masuala ya Utawala UNEP, wametangaza baadhi ya mambo yatakayojadiliwa, huku taifa la Kenya likizidi kupigia debe uhifadhi wa mazingira.

    Watu 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo la UNEA-6.

    #TV47Matukio

    Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.'

    *About TV47* 'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES. __ For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047. __

    Connect with us:

    Website: https://www.tv47.digital/ Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE Twitter: https://twitter.com/tv47news Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/ TikTok: https://www.tiktok.com/@tv47_ke Telegram: https://t.me/tv47_ke WhatsApp: 0797 047 047 __