Skip to main content
Skip to main content

Kubanduliwa kwa Gavana Mutai | Spika aagiza uchunguzi wa mfumo wa kupiga kura

  • | Citizen TV
    1,194 views
    Duration: 1:34
    Kesi ya kubanduliwa kwa gavana wa Kericho Dkt. Eric Mutai iliingia siku ya pili leo, wawakilishi wadi wakijikakamua kuwashawishi maseneta kumfurusha gavana huyo afisini, wakidai amepora mali ya umma na kutumia mamlaka yake vibaya. Hata hivyo, gavana Mutai alidai baadhi ya wawakilishi wadi walitumia njia ya mkato kumtimua, akidai mfumo wa kidijitali wa kupiga kura ulidukuliwa na kutumika vibaya kumfurusha. Spika wa bunge la seneti Amason Kingi sasa ametaka uchunguzi kufanywa na ripoti kufikishwa bungeni kuhusu mfumo huo wa kupiga kura