Kudhibiti sekta ya filamu | Kanuni mpya zatangazwa

  • | KBC Video
    113 views

    Bodi ya kuainisha filamu humu nchini itatoa ilani mnamo siku ya ijumaa tarehe 25th kwa lengo la kuhamasisha umma kuhusu uamuzi wake ulioafikiwa hivi majuzi wa kufafanua upya majukumu ya mawakala wa filamu humu nchini. Kwa mujibu wa uamuzi huo, kuanzia tarehe mosi mwezi Disemba mwaka huu, majukumu ya mawakala hayo yatawekewa masharti kadha ikiwemo kutoa usaidizi wa kiufundi kwa watayarishaji filamu na vipindi vya televisheni wa kigeni na kuhakikisha watayarishaji filamu wa kigeni wanazingatia sheria za humu nchini. Kaimu mwenyekiti wa bodi hiyo Christopher Wambua alisema bodi hiyo ina jukumu la kutoa leseni kwa watayarishaji filamu wa humu nchini moja kwa moja bila kuwahusisha mawakala.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #KFCB #News #filamu