Kundi la Police Reforms Working Group lataka dhuluma za polisi ziangaziwe

  • | Citizen TV
    400 views

    Kundi la Police Reforms Working Group sasa linamtaka Rais William Ruto kutoa ripoti kamili ya jopokazi lililoangazia mageuzi katika idara ya polisi na ile ya magereza wakidai kuwa masuala ya maafisa wa usalama kukiuka haki za kimsingi hayakuzingatiwa. Wakizungumza walipokutana katika afisi za tume ya kutetea haki za kibinadamu KHRC wanaharakati hao walisema kukosekana kwa masuala hayo katika ripoti hiyo ni kinyume cha katiba. Pia wametaka serikali kuweka mikakati dhibiti ya kukabiliana na visa vya ufisadi katika idara ya polisi.