Kizaazaa kilizuka katika eneo la Kamangu, eneo bunge la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu, baada ya kundi la wanawake kuvamia nyumba ya mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati anayedaiwa kuendeleza matumizi ya dawa za kulevya katika eneo hilo. Wanawake hao walitishia kuchukua sheria mikononi mwao ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa mara moja kukabiliana na tatizo hilo, wakisema uraibu wa dawa za kulevya umesababisha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoacha shule na utovu wa nidhamu miongoni mwa vijana wa eneo hilo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive