Kutoka Uigizaji hadi Utumishi wa Umma

  • | BBC Swahili
    707 views
    Ni muigizaji maarufu nchini Kenya, na wengi wanamfahamau kama ‘Baraza’ kutokana na kushiriki kwake katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha ‘Tausi’ kilichooneshwa karibu miongo miwili iliyopita. Lakini zaidi ya sanaa, Ken Ambani ameshika njia tofauti katika taaluma yake na sasa ni waziri katika serikali ya kaunti ya Mombasa ambapo anasimamia idara ya utawala wa huduma za jamii, vijana, jinsia na michezo. Ken anaelezea namna alivyoanza uigizaji hadi mabadiliko anayopitia kutoka kwenye kuigiza hadi utumishi wa umma. #bbcswahili #kenya #uigizaji