Kwa nini rais Ruto na rais mstaafu Uhuru Kenyatta waliteua walinzi wao kutoka kaunti ya Samburu

  • | Citizen TV
    6,065 views

    Hatua ya Rais William Ruto na Rais Mstafu Uhuru Kenyatta ya kuwateua walinzi wao yaani ADC kutoka Kaunti ya Samburu imeonekana kuipa hadhi mpya Kaunti hiyo ya wafugaji iliyo na sifa ya utovu wa usalama kutokana na wizi wa Mifugo na mauaji ya mara kwa mara. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alimteua mlinzi wake Timothy Lekolol huku Rais William Ruto akimridhia Fabian Letais Lengusuranga ambaye ni mzaliwa wa Baragoi jambo ambalo wakaazi wa Samburu wanajivunia.