Maafisa wa EACC wavamia makao ya mkurugenzi wa vyuo vya viwanda NITA

  • | Citizen TV
    1,644 views

    Maafisa wa upelelezi kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini EACC wamemkamata Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Viwanda (NITA) Stephen Ogenga katika uchunguzi unaoendelea wa madai ya utoaji wa zabuni ya zaidi ya shilingi milioni 28.4 kinyume cha sheria. Ogenga na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NITA Paul Kipsang Kosgei na washukiwa wengine wawili wanachunguzwa kuhusu madai ya kukiuka sheria kwa kutoa zabuni .