Maafisa wakuu wa usalama Garissa, waandaa mkutano kufuatika kukithiri kwa visa vya uhalifu

  • | Citizen TV
    68 views

    Katika mkutano uliowahuhisha viongozi wa kijamii na wakuu wa usalama, katika eneo la Garissa ilibainika kuwa matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana yamechangia kuongezeka kwa visa vya uporaji wa mali na kudorora kwa hali ya usalama. Aidha, wenyeji walitahadharishwa dhidi ya kuwaficha wahalifu miongoni mwao wakionywa kuwa wao pia watachukuliwa hatua. Wenyeji walipendekeza kujengwa kwa kituo cha polisi eneo hilo ili kukabiliana na utovu wa usalama.