Skip to main content
Skip to main content

Maandamano Embu

  • | Citizen TV
    2,862 views
    Duration: 1:58
    Mioto iliwashwa katika barabara kadhaa mjini Embu na maeneo ya karibu kufuatia mgomo unaoendelea nchini kulalamikia ongezeko la bei ya mafuta. Magari ya usafiri wa umma yaligoma huku shughuli za usafiri zikikwama kabisa Magari mengi yalikuwa yameegeshwa katika vituo kadhaa, wakazi wakilazimika kutembea kwa muda mrefu. wafanyibiashara pia walifunga maduka yao wakihofia ghasia huku maafisa wa usalama wakipiga doria mjini humo.. Katika mitaa kadhaa maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walizunguka kuzima mioto iliyokuwa imewashwa barabarani na kusababisha msongamano wa magari. Wenye bodaboda waliokuwa na nia ya kubeba abiria walizuiwa kufanya hivyo huku wakitakiwa kujiunga na wenzao kwenye mgomo..