- 30,606 viewsDuration: 28:03Wakaazi wa Minneapolis waliokuwa na hasira wamefanya maandamano baada ya afisa wa uhamiaji kumuua kwa kumpiga risasi mwanamke mmoja ambaye ni raia wa taifa hilo la Marekani. Renee Good mwenye umri wa miaka 37 alipigwa risasi kupitia kioo cha mbele cha gari lake. Rais Trump amesema Renee alikuwa amemkanyaga kwa gari afisa huyo wa uhamiaji lakini meya wa mji huo anasema kuwa afisa huyo alifanya hivyo kiholela na bila kujali. Mamia ya maafisa wa uhamiaji wametumwa Minneapolis katika juhudi za kupambana na uhamiaji haramu. #Minneapolis #Trump #ReneeGood #BBCSwahiliLeo #BBCSwahiliLeo #Trump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw