Maandamano yapangwa Mombasa kupinga uamuzi wa korti kuhusu usajili wa makundi ya ushoga na usagaji

  • | K24 Video
    78 views

    Uamuzi wa mahakama ya juu nchini ulioidhinisha kusajiliwa kwa mashirika ya kutetea haki za mashoga na wasagaji umezua hisia kali miongoni mwa viongozi wa dini na wabunge. Kamati ya bunge kuhusu utamaduni na michezo imeapa kuanzisha mikakati ya kuwasilisha mswada bungeni ambao utazuia utekelezwaji wa uamuzi huo na kupendekeza adhabu kali kwa watakaohusishwa na maswala hayo hapa nchini.